Dhamira Yetu

Kuhusu Fintantech

Fintantech ni jukwaa la elimu ya fedha linalolenga kuwawezesha Waafrika, hasa Watanzania, kupata maarifa sahihi ya uwekezaji na usimamizi wa fedha.

Kwa Nini Tulianza?

Chini ya asilimia moja (1%) ya Watanzania wanawekeza katika masoko ya mitaji. Hii ni kwa sababu wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu uwekezaji na usimamizi wa fedha. Fintantech ilianzishwa ili kuziba pengo hili.

Tunaamini kwamba elimu ya fedha ni silaha muhimu katika mapambano dhidi ya umasikini. Kupitia maandiko yetu, tunajaribu kufanya maarifa ya fedha kuwa rahisi kuelewa kwa kila mtu — haijalishi kiwango chake cha elimu.

Tunafanya Nini?

Tunaandika kuhusu mada mbalimbali za fedha ikiwa ni pamoja na:

  • Uwekezaji katika hisa — kuelewa masoko ya mitaji na jinsi ya kuwekeza
  • Mifuko ya uwekezaji wa pamoja — UTT AMIS na mingineyo
  • Value Investing — falsafa ya uwekezaji yenye tija
  • Elimu ya fedha — kuzalisha, kutunza, kupangilia, na kuwekeza pesa
  • Thamani halisi ya hisa — Intrinsic Value na Margin of Safety

Maono Yetu

Tunataka kuona jamii ya Waafrika wenye uhuru wa kifedha — watu wanaoweza kufanya maamuzi bora ya kifedha kwa sababu wana maarifa sahihi. Elimu ya fedha sio kwa wasomi pekee. Ni haki ya kila mtu.

Elimu ya fedha ni silaha muhimu katika mapambano dhidi ya adui umasikini.

Anza Safari Yako ya Kifedha

Jiunge nasi leo na upate maarifa ya bure kuhusu fedha na uwekezaji.

Jiunge SasaSoma Maandiko